Esteban Gutierrez:asajiliwa - Ferrari

Haki miliki ya picha AP
Image caption Esteban Gutierrez

Timu ya magari yendayo kwa kasi ya Ferrari imemsajili dereva Esteban Gutierrez kuwa dereva wa akiba wa timu hiyo.

Gutierrez mwenye miaka 23, raia wa Mexico alikua katika timu ya Subaru kwa miaka miwili na kufanya vizuri katika michuano ya Grand Prix msimu wa 2013.

Mkuu wa timu ya Ferrari Maurizio Arrivabene

amemuelezea dereva huyo mpya" ingawa bado ni kijana ila ni mzoefu wa mambo mengi katika kizazi kipya cha magari ya F1".

Huku Gutierrez akielezea ni "Ni mwanzo wangu wa kwenda mbele na kufanya makubwa, kwa kuchangia mafaniko na malengo yaliyowekwa".

Madereva wakuu wa timu ya Ferrari kwa msimu ujao ni Sebastian Vettel, na Kimi Raikkonen.