Sijawahi panga matokeo : Herrera

Haki miliki ya picha AP
Image caption Andre akiwa kazini.

Kiungo wa timu ya Manchester United Ander Herrera amesisitiza hajawahi kupanga matokeo ya mechi wakati akiichezea klabu Real Zaragoza.

Mhispania huyu ametajwa katika kundi la wanamichezo 41 wakiwemo wachezaji ,makocha na wakurugenzi katika uchunguzi wa kashfa ya upangaji matokeo kwenye ligi kuu ya Hispania.

Herrera ameandika katika ukurasa wake wa facebook.:Sijawahi na kamwe sintofanya chochote katika kupanga matokeo,naupenda mpira naamini katika mchezo wa haki nje na ndani ya uwanja:

Waendesha mashitaka wanadai fedha taslimu € 965,000 zililipwa kwa kocha Javier Aguirre na wachezaji tisa wa Zaragoza, ikiwa ni pamoja na Herrera, kabla ya mchezo wa La Liga mwishoni mwa msimu wa 2010-201.

Herrera aliondoka Zaragoza na kujiunga na timu ya nyumbani kwao ya Athletic Bilbao mwezi Agosti 2011, kabla ya kujiunga na Man United mwezi Juni 2014.