Bondia Anthony Crolla Alazwa

Image caption gloves za boxing

Bondia wa Uingereza Anthony Crolla amepelekwa hospitali baada ya kupata majeraha makubwa kichwani na kuvunjwa kifundo cha mguu.

Crolla, mwenye miaka 28, alipelekwa Hospitali ya Royal Oldham iliyoko mjini London, na anasubiri kufanyiwa vipimo Zaidi.

Hali hii imepelekea kuahirishwa kwa mchezo wake iliokua umepangwa kuchezwa Januari 23 mwaka 2015 ambapo alikua azipige na bondia Richar Abril.

Akizungumza promota wa Crolla Eddie Hearn alisema “Ilikuwa ndoto yake kupata ubigwa wa dunia. Nimewambia timu Abril na tunaimani tunaweza kupanga upya. Hatujajua kiwango cha majeruhi yake. afya yake ni wasiwasi wetu wa kwanza kwa sasa”.

Anthony Crolla ni bondia wa uzito mwepesi amepigana jumla ya mapambano 35 na kushinda 29 huku akishinda mapambano 10 kwa KO akipoteza michezo 4 na kwenda sare mara mbili.