Northampton yaongeza mikataba-wachezaji

Timu ya rugby ya Northampton imeongeze mikataba kwa nyota wake saba wakiongozwa na wachezaji pacha wawili wa Uingereza Dylan Hartley and Courtney Lawes.

Wachezaji wengine waliongeza kandarasi ya kuendelea kuitumikia timu hiyo ni pamoja na Calum Clark,Alex Waller, Ethan Waller, James Craig and Gareth Denman.

Nahodha Hartley amekataa kujiunga na timu ya Montpellier ya Ufaransa waliokuwa wakimuwania,amesaini mkataba wa miaka mitatu unaomuweka hapo kwa misimu 13.

Nyota hawa wanatarajiwa kuisaidia timu kuendelea kufanya vizuri kwenye ligi ya rugby.