Mchezaji Ebosse alipigwa,ripoti yasema

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Albert Ebosse aliyefariki baada ya kupigwa.

Matokeo ya uchunguzi wa mwili wa mchezaji soka wa Cameroon Albert Ebosse aliyefariki nchini Algeria yamebaini kwamba mwanasoka huyo aliuawa baada ya kuvamiwa na kupigwa katika eneo la kubadilishia jezi na wala hakuuawa kwa kupigwa na kitu katika kichwa chake.

Mchezaji huyo wa kilabu ya JS Kabylie alifariki mwezi Agosti baada ya timu yake kufungwa.

Matokeo ya uchunguzi ulifanywa na serikali ya Algeria ulibaini kwamba mchezaji huyo wa miaka 24 aliuawa baada ya kupigwa na kitu katika kichwa chake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mchezaji wa JC Marehemu Albert Ebosse

Lakini uchunguzi uliofanywa na mtaalam anayechunguza chanzo cha kifo kufuatia ruhusa iliotolewa na familia yake,umesema kuwa kifo chake kinatokana na uvamizi wa kikatili dhidi yake katika eneo la kubadilisha jezi.

Wakati huo,waziri wa michezo nchini humo Mohammed Tahmi alisema kuwa Ebosse alifariki baada ya kupigwa na kitu katika kichwa, kisa hicho kilichosababisha kilabu hiyo ya Kabylie kupigwa marufuku kwa miaka miwili katika mashindano yoyote ya bara Afrika na kulazimishwa kucheza mechi zake za nyumbani bila mashabiki.

Lakini matokeo ya uchunguzi wa Andre Moune yamesema kuwa kulikuwa na mvutano wakati wa uvamizi huo ,ambapo Ebosse alipigwa ngumi katika kichwa chake ilioathiri fuvu lake la kichwa.