Real, San Lorenzo nani Bingwa wa dunia?

Haki miliki ya picha AP
Image caption San Lorenzo na furaha ya ushindi

Klabu ya San Lorenzo ya Ajentina wamefanikiwa kufuzu kucheza fainali yak kombe la dunia kwa vilabu baada ya kupata ushindi kwa kuilaza Auckland City 2-1 katika mchezo uliochezwa dakika 120.

San Lorenzo ndio walianza kupata bao la dakika ya 45 lilofungwana na kiungo Pablo Barrientos kabla ya akiwa Angel Luis Berlanga kuisawazishi Auckland City kwa goli la dakika ya 67.

Mshambuliaji Mauro Matos aliwahakishia San Lorenzo nafasi ya kwenda fainali kwa goli lake la dakika ya 93 katika dakika za nyongeza za mchezo.

Kwa ushindi huo San Lorenzo ya nchini Ajentina watawakabali miamba wa ulaya Real Madrid katika mchezo wa fainali.