Aston Villa kuipinga kadi ya Gabby

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aston Villa

KLABU ya Aston Villa imethibitisha itakata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Mchezaji wao Gabby Agbonlahor.

Agbonlahor alipewa kadi nyekundu dakika 65 ya mchezo baada ya kuonekana amemchezea rafu mchezaji Ashley Young wa Manchester United.

Mara baada ya Mechi hiyo, Meneja wa Villa, Paul Lambert, alikaririwa akisema kuwa Agbonlahor hakustahili kutolewa na pia kudai Ashley Young alimwambia Kipa wa Villa Brad Guzan kwamba yeye ndie alimchezea Rafu Agbonlahor.

Hii ilikua ni kadi ya pili mfululizo kupata kwa wachezaji wa Aston Villa baada ya kiungo Kieran Richardson kupewa kadi dhidi West Bromwich Albion katika mchezo uliopigwa Desemba 13.

Agbonlahor atakosa michezo mitatu ya ligi kuu kama rufaa yao itakataliwa na chama soka cha England FA.