Azam fc kuanza na El Merreikh

Image caption Timu ya Azam Fc

Mabingwa Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2013/14 , Azam FC wamepangwa kucheza na Timu ya El Merreikh ya Sudan.

Mechi hiyo ya Ligi wa Mabingwa Afrika itakuwa ya kwanza kwa Azam FC katika kampeni zao za kuwania na kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hii ni mara ya kwanza timu hiyo kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa ya Caf ni kwamba Azam FC itaanzia nyumbani Dar es Salaam na kumalizia ugenini mechi ya pili mjini Kharthoum.

Wakati huo huo Timu ya Yanga itaanza kampeni yake ya Kombe la Shirikisho kwa kuivaa BDF IX ya Botswana inayomilikiwa na Jeshi la nchi hiyo.

Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetangaza ratiba ya michuano hiyo.

Yanga itaanzia nyumbani na kumalizia ugenini dhidi ya Waswana hao waliowahi kung'olewa na Timu ya Simba.