Mwaka huu kamwe sitausahau - Carlo Ancelotti

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Furaha ya mwaka wa ushindi 2014

Kocha wa Real Madrid mwitaliano Carlo Ancelotti amesema kitendo cha klabu yake kushinda taji la klabu bingwa dunia kimeifanya klabu hiyo kuumaliza vyema mwaka 2014 kwa kufanikiwa kushinda mataji manne ndani ya mwaka mmoja.

Mabingwa hao wa ulaya walifanikiwa kuwafunga mabingwa wa bara la Amerika Kusini San Lorenzo mabao 2-0 na kufanikiwa kutwaa taji hilo nchini Morocco.

Makombe mengine ya Real mwaka huu ni Champions League, Copa del Rey na Uefa Super Cup.Ancelotti amesema wamefanya vizuri mwaka huu na kamwe hautasahaulika,umoja wa timu yake ni kama familia.

Real Madrid imefanikiwa kufunga jumla ya magoli 178 kwenye mashindano yote na kuweka rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye mwaka mmoja.