Mohammed Ali anaendelea vyema .

Image caption Nguli wa zamani wa masumbwi Muhammad Ali

MSEMAJI wa nguli wa zamani wa masumbwi Muhammad Ali amedai kuwa hali ya bondia huyo inaendelea vyema toka alazwe hospitalini hapo kwa maradhi ya maambukizi katika mapafu.

Msemaji Bob Gunnell amesema madaktari wanaomtibu Ali wana matumaini ya kumruhusu katika kipindi cha karibuni.

Gunnell aliendelea kudai kuwa familia ya nguli huyo bado inaomba suala hilo kuachwa kuwa la binafsi na kushukuru maombi yote ya kumtakia heri.

Ali mwenye umri wa miaka 72 bingwa wa wa zamani mara tatu wa uzito wa juu duniani ambaye anaugua ugonjwa wa kutetemeka au Parkinson alikimbizwa hospitali Jumamosi iliyopita.

Ali aligundulika kuwa na Parkinson mwaka 1984, miaka mitatu baada ya kutangaza kustaafu masumbwi.