Woods asubiri msimu mpya kwa hamu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Tiger Woods

Mchezaji wa gofu Tiger Woods ameonyesha furaha baada ya kukabiliana na matatizo ya maumivu.

Wood aliyewahi kuwa mchezaji namba moja wa mchezo huu amekua akisumbulia na maumivu ya mgongo kwa miaka ya hivi karibu.

Mchezaji huyo alirejea uwanjani katika michezo ya Dunia ya gofu amekua na shauku ya kufanya vizuri kuanzia mwaka 2015.

"Mimi nina msisimko zaidi kwa kuwa na afya njema tena nimefanya jitahada katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuikabili hali hii”.

Tiger Woods ameshangazwa na namna alivyoweza kurudi mchezoni na msaada aliokua anapata.