Ramsey kuivaa Southampton.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arsene Wenger kocha wa Arsenal

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa nahodha wake Mikael Arteta atachelewa kidogo kupona majeruhi yanayomsumbua lakini kiungo Aaron Ramsey anaweza kuwa fiti kwa ajili ya mchezo dhidi ya Southampton wakati wa mwaka mpya.

Arteta alipata majeruhi mwezi uliopita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund.

Wenger amesema nahodha wake huyo anaendelea vyema lakini atachelewa kidogo kuliko ilivyotegemewa lakini Ramsey anaweza kurejea katika mchezo dhidi ya Southampton.

Ramsey alikuwa akirejea katika kiwango chake cha msimu uliopita akiwa amefunga mabao matatu katika mechi mbili kabla ya kutolewa wakati wa mapumziko katika mchezo dhidi ya Galatasaray mapema mwezi huu.

Wenger pia amebainisha kuwa Laurent Koscielny naye anakaribia kurejea katika kikosi cha kwanza na anaweza kuwepo katika kikosi chake kitakachopambana na West Ham United huko Upton Park.