Loic Courteau kujiunga na Andy Murray?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Andy Murray

Kocha wa mchezo wa tenesi anafanya mazungumzo ya kujiunga na timu ya Andy Murray msimu ujao.

Loic Courteau mwenye miaka 50, amekua kocha wa nyota mwingine wa tenesi Amélie Mauresmo kwa kipindi cha mika sita.

"Ni changamoto ya kuvutia kufanya kazi na timu ya Murray siwezi kukata kwenda kufanya nao kazi "

Murray alimtimua kocha wake Dani Vallverdu,pamoja mkufunzi wa mazoezi ya viungo Jez Green

Huenda Courteau akawa kocha wa timu ya Murray kabla kuanza msimu mpya wa michezo ya tenesi huko Abu Dhabi.