Bolton yamsajili mgongwe Heskey

Image caption Emile Heskey mwenye nguo nyeupe akiwa kazini.

Klabu ya Bolton Wanderers imetangaza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Emile Heskey kwa mkataba wa muda mfupi.

Heskey mwenye umri wa miaka 36 amekuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo huku akikitumikia kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 katika mchezo dhidi ya Reading Jumatatu iliyopita.

Mkongwe huyo ambaye ameitumikia Uingereza mechi 62 alikuwa akicheza katika klabu ya Newcastle Jets ya Australia ambayo ilimuachia April mwaka huu.

Bolton kwasasa inasubiri ITC ya mshambuliaji ili kukamilisha usajili wake.