Ivory coast wagomea bajeti ya serikali –afcon

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Timu ya Ivory Coast

Shirikisho la soka Ivory Coast (FIF) limegomea bajeti waliyopewa na Serikali ya nchi hiyo kwa ajili ushiriki wa timu ya taifa, The Elephants kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kwa sababu ni ndogo.

Serikali imekubali kutoa dola za Kimarekani 575 805 kwa Tembo wa Ivory Coast kwenye Fainali za AFCON zitakazofanyika Equatorial Guinea kuanzia Januari 17 hadi Februari 8.

Pamoja na hayo, Makamu wa rais wa FIF, Sory Diabate amewaambia Waandishi wa Habari kwamba Hawawezi kwenda CAN (Mataifa ya Afrika) na faranga (za Ivory Coast, CFA Francs) Milioni 310. Kwa kuwa wamewasilisha bajeti yao kwa ufafanuzi mzuri.

Waziri wa Michezo wa nchi hiyo alikuwa tayari kutoa fungu kamili waliloombwa katika bajeti ya awali faranga bilioni 3.5, pamoja na hayo Ivory Coast ilikwenda michuano hiyo mwaka 2013 Afrika Kusini na jumla ya Faranga bilioni 3.9, huku Serikali ikichangia Bilioni 2.7 wakati Tembo walitolewa na Nigeria katika Robo Fainali.

Kikois cha Herve Renard, kitaanza maandalizi yake kwa kuweka kambi Abu Dhabi, Falme za Kiarabu Januari 5, mwakani. Ivory Coast imepangwa Kund D pamoja na Mali, Cameroon na Guinea.