Matic asema Chelsea itashinda mataji 4

Image caption Kiungo wa kati wa Chelsea Nemanja Matic amesema kuwa timu hiyo itashinda mataji yote manne inayopigania

Mchezaji wa kilabu ya Chelsea Nemanja Matic amesema kuwa anaamini kuwa kilabu hiyo itashinda mataji manne msimu huu.

Hakuna kilabu ambaye imefanikiwa kushinda taji la ligi ya Uingereza,taji la kilabu bingwa barani Ulaya,taji la shirikisho la Ligi ya Uingereza FA na lile la ligi ya Uingereza.

Lakini Matic ambaye alijiunga tena na Chelsea kutoka Benfica kwa kitita cha pauni 21 mwezi Janauari amesema kuwa anaamini inawezekana.

Viongozi hao wa ligi ya EPL wako katika semi fainali ya kombe la Capital cup,wako katika timu 16 za kombe la vilabu bingwa ulaya na bado hawajaanza kampeni ya kombe la shirikisho la Uingereza FA.

Matic anasema kuwa: tuna ubora na imani ,ninaiamini timu yangukwa hivyo hakuna lisilowezekana.

Meneja Jose Mourinho tayari amesema kuwa hana uhakika wa chelsea kushinda mataji manne msimu huu.