Zambia yataja kikosi cha AFCON 2015

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Timu ya taifa ya Zambia

Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zambia Honor Janza ameteua kikosi kipya ambacho kina jumla ya wachezaji 27 kwaajili ya kushiriki katika fainali za Mataifa huru ya Afrika mwaka 2015 .

Janza amewaita wachezaji 12 walioshiriki AFCON ya mwaka 2013 na wachezaji 11 kutoka kikosi kilichotwaa kombe hilo mwaka 2012.

Makipa: ni kennedy Mwene (Mamelod Sundowns) Danny Munyau (Red Arrows) Toaster Nsabata (nchanga Rangers)Joshua Titima (Power Dynamos).

Mabeki:Stopila Sunzu(Sochaux, France) Bronson Chama(Red Arrows) Donashani Malama(Nkana)Aaron katebi ( Fc platinum ,zimbabwe) Christopher Muntali (Nkana)Emmanuel mbola(Hapoel Raana ,Israel)Davie Nkausu(Bloemfotein celtic ,RSA)Rodrick Kabwe (Zanaco)

Viungo:Nathani Sinkala(Grasshoppers swazland ) Chisamba Lungu(Fc ural Russia)Mukuka mulenga(Bloemfotein)Kondwani Mtonga (North east Utd) Spencer sautu (Green Eagle)Rainford kalaba(Tp Mazembe ,DRC) Bruce musakanya( Red Arrows) Lubonda Musonda(Fc lusses, Armenia)

Washambuliaji:Emmanuel Mayuka(southampton, England)Given singuluma(Tp mazembe DRC)Ronald sate sate kampamba(Nkana)Evance kangwa(Hapoel Ra anana,Israel(Patrick ngoma(Red Arrows)Jackson mwanza (Zesco utd) na James Chamanga( Liaonng whowin,China)

Timu hiyo itaingia kambini desemba 26 na inataraji kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na Bafana bafana Januari 4.