EPL:Meneja wa WBA ahofia hatma yake

Image caption Kocha wa West Bromwich Alan Irvine anayehofia hatma yake baada ya misururu ya matokeo mabaya katika kilabu hiyo

Kocha wa West Bromwich Albion Alan Irvine anahofia hatma yake katika kilabu hiyo baada ya kichapo cha mabao 3-1 walichopata kutoka kwa Mancity.

Matokeo hayo yaliiwacha kilabu hiyo na alama mbili juu ya eneo la kushushwa daraja baada ya kushinda mechi mbili pekee katika mechi 12.

Baada ya kufutwa kwa Neil warnock wa Crystal palace,Irvine ni meneja mwengine ambaye huenda akapigwa kalamu .

Hatahivyo meneja huyo amesema kuwa mwenyekiti wa kilabu hiyo atatoa uamuzi kuhusu hali hiyo.

''Siwezi kuidhibiti'',alisema Irvive.

Irvine mwenye umri wa miaka 56 alitajwa kuwa meneja wa kilabu hiyo baada ya kuondoka kwa Pepe Mel mnamo mwezi June.