Harakati za Man U zafifia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption nahodha wa kikosi cha Man U wayne rooney baada ya timu hiyo kupata sare ya 0-0 dhidi ya Totenham

Harakati za Manchester United kujaribu kuwafikia Chelsea na mabingwa wa ligi hiyo Mancity zilipata pigo baada ya kupata sare ya 0-0 dhidi ya Totenham Hotspurs.

United ilitengeza nafasi nyingi za wazi katika kipindi cha kwanza huku shambulizi la Juan Mata likipiga chuma cha goli.

Hatahivyo mlinda lango wa Totenham Hugo Lloris alilazimika kufanya kazi ya ziada baada ya kuwanyima mabao Radamel Falcao,Robin Van Persie na Ashley Young.

Kiungo wa kati wa Spurs Andros Townsend alifanya mashambulizi makali katika ngome ya manchester United huku Ryan Mason akikosa bao la wazi katika dakika za mwisho.

Kikosi hicho cha Mauriccio Pochettino kimekuwa kikifunga mabao yake katika dakika za lala salama dhidi ya Swansea na Leicester lakini licha ya kudhibiti mpira dakika 15 za mwisho katika kipindi cha pili hawakuweza kupata bao.