Kambi ya Kriketi yaanza leo Tanzania

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Timu ikichakarika

Timu ya taifa ya Tanzania inaanza kambi leo Dar es Salaam kujiandaa na michuano ya kriketi ya Afrika chini ya miaka 19 daraja la 1 itakayofanyika nchini Namibia mapema mwakani.

Kambi hiyo chini ya kocha mchezaji Hamis Abdallah inakuja baada ya majuma mawili ya michuano ya majaribio yaliyofanyika Nairobi, Kenya huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu baada ya wenyeji kuwafunga Uganda.

Namibia itakuwa wenyeji wa michuano hiyo itakayokuwa ni sehemu ya kufuzu kucheza kombe la dunia chini ya miaka 19.

A wali michuano hiyo ilipangwa kuanza Januari Mosi na kupelekwa mbele hadi Februari.

Kenya na Uganda zitakuwa miongoni mwa nchi shiriki kutoka Afrika Mashariki na michuano ya Nairobi ilikuwa na lengo la kuziandaa timu zao.

Abdallah ameiambia BBC kuwa baada ya mapumziko ya Christmas wanaanza mazoezi wakiwa na ari na nguvu.

Timu ya Tanzania hivi karibuni ilichukua ubingwa Wa Afrika chini ya miaka 19 ligi daraja la 2, hivyo kufuzu michuano ya Namibia itakayoanza mapema mwezi wa pili