Mourinho alaumu vyombo vya habari na waamuzi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jose Mourinho

Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho anaamini kuwa kuna kampeni zinaendelea kuwashawishi waamuzi kutoa mamuzi tofauti dhidi ya timu yake.

Mourinho amekasirishwa na mwamuzi Anthony Taylor kwa kushindwa kutoa penati katika mchezo dhidi ya Southampton ulomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kiungo Cesc Fabregas alipewa kadi ya njano baada ya kuanguka katika eneo la hatari la Southampton, kwa kukwatuliwa na Matt Target na kuoneka na kama amemuhadaa mwamuzi kwa kujiangusha.

Baada ya mchezo huo Mourinho alilamika kuwa vyombo vya habari, watangazaji mameneja wa timu zingine wote wanatoa shinikizo kwa waamuzi hivyo anadhani kuna kampeni inaoendelea dhidi ya timu yake.

"Sijui kwa nini kuna kampeni inaendelea dhidi ya timu yangu ila sijali,kila mtu anajua ile ilikua ni penati."

Mourinho anafahamika Zaidi kwa kwa kauli zake tata ambazo amekua akizitoa mbele ya waandishi wa habari.