Phil Taylor atinga raundi ya tatu.

Image caption ubao wa mchezo wa vinyoya

Mshindi mara kumi na sita wa dunia kwa mchezo wa kurusha vishale Phil Taylor, amefanikiwa kuingia hatua ya tatu ya mchezo vishale ya dunia .

Phil Tayloar ameibuka kidedea baada ya kumshinda mpinznia wake Mark Websterkwa ushindi wa 4-0.

Mchezaji huyu anashika nafasi ya pili kwa ubora duniani akielezea mchezo huo"Ulikua mchezo mgumu Mark alinipa changamoto ila nimemaliza vizuri hicho ndio cha muhimu".

Taylor mwenye miaka 54,atachuana na Kim Huybrechts wa Ubeligiji aliemfunga Kevin Painter kwa 3-1.

Huku katika michezo mingine Adrian Lewis liibuka na ushindi wa 4-2 dhidi Keegan Brown, Andy Hamilton4 - 2Kyle Anderson na Cristo Reyes akimtungua 4 - 3Kevin Painter.