Timu nane zaTennis kuchuana Tanzania

Image caption Binti akirudisha majibu mchezoni

Timu kutoka nchi za Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Shelisheli, Sudan, visiwa vya Comoro zitashindana nchini Tanzania hapo mwakani katika michuano ya tennis ya Afrika kwa watoto chini ya miaka 12, 14 na 16.

Shirikisho la tennis Tanzania (TTA) limesema lipo tayari kwa uwenyeji katika michuano hiyo itakayochezwa kuanzania January 11-19 katika viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.

Kocha Majuto Majaliwa, anayetambulika na shirikisho la tennis duniani (ITF) amesema wachezaji wa Tanzania wataanza mazoezi Jumamosi ili kujiweka tayari.

“Tumechagua timu yenye wachezaji wazuri ambao wataweza kuipeperusha bendera ya Tanzania nyumbani”.

‘Kuwa wenyeji ni furaha kwetu kwa sababu wachezaji watakuwa wakicheza nyumbani katika viwanja walivyovizoea”, alisema Majaliwa.

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kuandaa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.