Lallana ,Moreno waibeba Liverpool

Haki miliki ya picha PA
Image caption wachezaji wa tiumu ya Liverpool kushoto ni Phellippe Coutinho,Luis Suares,na Steven Gerrard.

Majogoo wa jiji liverpool wakicheza katika uwanja wao wa Anfield wameibuka na mshindi wa kishindo kwa kuichapa Swansea mabao 4-1.

Beki Alberto Moreno alikuwa wa kwanza kuipatia liverpool goli la kwanza dakika ya 33,kiungo Adam Lallana akaongeza mabao mawili dakika ya 51 na 61, Shelvey Jonjo akajifunga dakika ya 69 na kuwahakikishia majogoo ushindi.

Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Swansea lilifugwa na kiungo mshambuliaji Gylfi Sigurdsson.

Kwa ushindi huo liverpool wanashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi wakiwa wameshuka dimbani mara 19.