Tuzo za Caf kutolewa Januari

Image caption Pierre-Emerick Aubameyang

Shirikisho la soka barani Afrika CAF litatoa tuzo kwa wanamichezo bora Januari 8 huko Lagos Nigeria.

Kiungo wa Gaboni Pierre-Emerick Aubameyang, golikipa Vincent Enyeama wa Naijeria na kiungo Yaya Toure ndio wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2014.

Wanaowania Tuzo za uchezaji bora kwa wachezaji wa ndani ya Afrika

Akram Djahnit (Algeria) El Hedi Belamieri( Algeria)Firmin Mubele Ndombe (DR Congo)

Kwa upande wa wanawake wanaowania tuzo hizo ni

Annette Ngo Ndom (Cameroon) Asisat Oshoala (Nigeria) Desire Oparanozie (Nigeria)

Wanaowania kwa upande wa chipukizi

Asisat Oshoala (Nigeria) Fabrice Ondoa (Cameroon)Uchechi Sunday (Nigeria)

Wanaowania tuzo ya kipaji kinachochipukia ni

Clinton N’jie (Cameroon) Vincent Aboubakar (Cameroon) Yacine Brahimi (Algeria)

makocha wanaowania tuzo hizo

Florent Ibenge (DR Congo) Kheireddine Madoui (ES Setif) Vahid Halilhodžić (kocha wa zamani wa Algeria)

Timu zinazowania tuzo ya timu bora ya mwaka ni

Algeria, Libya, Nigeria

Timu bora ya wanawake ya Mwaka ni

Cameroon, Nigeria, Nigeria U-20

Klabu bora ya Mwaka

Al Ahly (Egypt) AS Vita (DR Congo) ES Setif (Algeria)

Huku Rais wa Tp Mazembe Moise Katumbi Chapwe akitarajiwa kupewa tuzo ya kiongozi bora wa michezo wa mwaka.