Arsenal yamlenga Carvalho na Sissoko

Image caption Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon William Carvalho anayelengwa na Arsenal.

Arsenal wanadaiwa kumfukuzia William Carvalho.

Kiungo huyo wa kati wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 22 anaweza kucheza katika safu ya kati ya ulinzi na amekuwa akilengwa na Gunners kwa mda mrefu licha ya kuwa na bei ghali.

Kilabu ya Sporting Lisbon inataka kitita cha pauni millioni 30 ,lakini kulingana na gazeti la daily mail nchini Uingereza kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kulipa pauni 25.5.

Vilevile Wenger ameripotiwa kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Newcastle Moussa Sissoko kwa kitita cha pauni millioni 9.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Moussa Sissoko wa Newcastle

Wakati huohuo meneja wa Manchester City Manuel Pelegrini anatarajiwa kumununua mshambuliaji wa Swansea Wilfried Bonny ili kuchukua mahala pake Sergio Aguero ambaye ana jereha la mguu.

Gazeti la Daily Telegraph limeripoti kuwa Manchester City pia inajiandaa kumnunua mshambuliaji huyo kwa takriban pauni millioni 30.

Hatahivyo kulingana na The Times ,Chelsea pia inamtaka mshambuliaji huyo.