Bush mwengine ataka urais Marekani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeb Bush ni mwana wa rais George Bush na nduguye ya George W Bush waliokuwa marais wa Marekani

Aliyekuwa Gavana wa Florida kupitia tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani Jeb Bush ameripotiwa kujiuzulu kutoka nyadhfa zake zote za bodi akijiandaa kuwania urais mwaka ujao.

Gazeti la The WashingtonPost limenukuu ujumbe wake kutoka kwa msaidizi wake uliodai kwamba bwana Bush pia amejiuzulu katika bodi ya hazina yake ya elimu.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 61 pia alitangaza mwezi uliopita kwamba alikuwa na wazo la kutaka kuwania wadhfa huo mkuu ambao hapo mbeleni ulishikiliwa na babaake George Bush na nduguye George W.

Amesema kuwa atafanya uamuzi wa mwisho baada ya kubaini iwapo ana ufuasi wa kutosha.