Southampton kumaliza juu ya Arsenal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha wa Southampton Ronald Koeman

Meneja wa kilabu ya Southampton nchini Uingereza Ronald Koeman anaamini kuwa kikosi chake kinaweza kumaliza msimu huu wa ligi kikiwa juu ya Arsenal na hivyobasi kupata fursa ya kushiriki katika kombe la vilabu bingwa barani ulaya.

Southampton kwa sasa wako nafasi ya nne juu ya Arsenal kwa tofauti ya mabao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachezaji wa kilabu ya Arsenal wakisherehekea bao lao

Timu hizo mbili zinakutana katika uwanja wa St. Marys siku ya Alhamisi,na alipoulizwa iwapo Southampton inaweza kumaliza juu ya The Gunners alijibu''Ninafikiria hivyo ,ninaamini tunaweza kupigania nafasi ya juu katika ligi'',.

Kilabu hiyo ilifanya vyema katika raundi ya kwanza ya ligi ya EPL licha ya kutia kitita cha pauni millioni 97.6 baada ya kuwauza wachezaji wake Adam Lallana,Luke Shaw na Dejan Lovren wakati wa msimu wa joto.