Mchezaji wa Anzi Makhachkala auawa Urusi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa timu ya taifa nchini Urusi

Gasan Magomedov mwenye umri wa miaka 20 anayeichezea kilabu ya Urusi Anzi Makhachkala ameuawa kwa kupigwa risasi karibu na nyumbani kwake kazkazini mwa Caucusus nchini Urusi.

Mogomedov alikuwa akiendesha gari lake wakati wa mfyatuliano wa risasi ndiposa gari lake likamiminiwa risasi na kumpelekea kuaga dunia kutokana na majeraha aliopata wakati alipokuwa akisafarishwa hospitalini.

Kulingana na kilabu hiyo ya Anzhi hakuna mtu aliyekamatwa na sababu ya tukio hilo haijulikani.

Kilabu hiyo imetuma rambirambi zake kwa familia ya Magomedov,mchezaji wa kiungo cha kati.

Hakuna ripoti za majereha mengine kufuatia kisa hicho.