Makamu wa Rais wa Fifa, Blatter kuchuana

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ali Bin Al Hussein atapambana na Rais wa Fifa Sepp Blatter kuwania Urais

Makamu wa Raisi wa Chama cha Soka dunia Fifa Ali Bin Al Hussein atachuana na bosi wake Sepp Blatter katika kuwania kiti cha urasi.

Ali mwenye miaka 39 atasimama kuwania uraisi kwenye uchaguzi utakaofanyika Mei 29 ambapo Blatter atakua akiwania kuongoza chama hicho kwa muhula wanne.

“Ni wakati wa kubadili mwelekeo wa kiutawala mbali na matatizo ya kimichezo vichwa vya habari viwe kuhusu soka sio Fifa" alieleza Ali.

Jerome Champagne, aliejiunga na Fifa mwaka 1999, akiwa ni balozi nae amedhibitisha kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi.

Wagombea wanaotaka kuwania nafasi za uongozi wanatatakiwa kutangaza nia kabla ya Januari 29.