Mzunguko wa nne kombe la FA hadharani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Manchester United kukipiga na Cambridge United

Droo ya kupanga mechi za raundi ya 4 ya Kombe la FA imefanyika kwa vigogo Manchester United kupangwa kucheza na timu ya daraja la chini ya Cambridge United.

Mabingwa Watetezi, Arsenal, watakuwa Ugenini kucheza na Brighton au Hove Albion ambayo ipo Daraja la chini ya Ligi Kuu England.

Chelsea itakipiga na Mill wall auBradford City Manchester City itapepetana na Middlesbrough

Southampton/Ipswich na Crystal Palace

Blackburn Rovers na Swansea City

Preston North End na Sheffield United

Birmingham City dhidi ya West Bromwich Albion

Aston Villa na Bournemouth

Cardiff City na Reading

AFC Wimbledon/Liverpool na Bolton Wanderers

Burnley/Tottenham Hotspur na Leicester City

Rochdale v Stoke City

Sunderland na Fulham/Wolves

Doncaster/Bristol City na Everton/West Ham

Michezo ya raundi nne inatarajiwa kupigwa Januari 24 na 25.