Simba yatinga nusu Fainali ya Mapinduzi

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Vijana wa timu ya Simba yenye makao yake makuu Msimbazi jijini Dar es Salaam

katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar, timu ya Simba imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuichakaza Taifa Jang'ombe mabao 4-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa jana usiku mjini Zanzibar. Michezo mingine ya robo fainali inaendelea leo kwa timu za KCC ya Uganda kumenyana na Polisi Zanzibar, Azam ya Tanzania itakwaruzana na Mtibwa Sugar pia ya Tanzania, huku Yanga ikikamilisha michezo ya hatua hiyo kwa kupambana na JKU ya Zanzibar saa mbili usiku mjini Zanzibar.