Mancity yakaribia kumsajili Bony

Haki miliki ya picha gett
Image caption Mchezaji Wilfried Bony wa Swansea

Usajili wa mshambuliaji wa Ivory Coast na Swansea Wilfired Bony hadi kilabu ya Mancity unakaribia kukamilika.

Ajenti wake anatarajia kwamba mkataba huo utawekwa sahihi wiki hii baada ya vilabu vya Swansea na Mancity kujadiliana kuhusu kitita cha fedha kinachotarajiwa kutolewa kumnunua mchezaji huyo.

Swansea wanataka pauni millioni 30 kwa mshambuliaji huyo ambaye amenukuliwa akisema kuwa ''ni vizuri iwapo Manchester City wanamuhitaji''.

Kila mchezaji angependa kucheza katika ligi ya mabingwa.

Image caption Mkufunzi wa Manchester City Manuel Pelegrini

Mwenyekiti wa Manchester City Khaldoon Al-Mubarak angependelea kutoa kitita cha pauni millioni 24 kwa mchezaji huyo.

Hatahivyo City ilithibitisha jana usiku kwamba hakuna kiwango cha fedha kilichoafikiwa,lakini mazungumzo kati ya vilabu hivyo viwili yalipangwa kufanyika katika kipindi cha masaa 24 ili kupata mwafaka.

Mkufunzi wa City Manuel Pellegrini anataka kuimarisha safu yake ya mashambulizi ili kutetea taji lao.