Fabregas:Messi hawezi kuondoka Barcelona

Image caption Messi kushoto akiwa na Fabregas katika kilabu ya Barcelona

Mchezaji wa kiungo cha kati katika kilabu ya Chelsea Cesc Fabregas anaamini kwamba Lionel Messi hataondoka katika kilabu ya Barcelona.

Chelsea imehusishwa na mchezaji huyo kufuatia madai kwamba amekuwa akizozana na Kocha Luis Enrique.

Lakini Fabregas ambaye ni rafiki wa karibu wa mchezaji huyo wa Argentina hafurahii madai ya vyombo vya habari kwamba anajaribu kumshawishi Messi kujiunga na The Blues.

''Messi anafurahia kuwa Barcelona na Barcelona inafurahia kuwa naye'',alisema mchezaji huyo wa Uhispania.

''Nimeshangazwa kwamba mimi najaribu kumvuta Messi katika kilabu ya Chelsea kwa niaba ya Chelsea,nitawezaje kuzungumza kuhusu kandarasi na mimi ni mchezaji tu''.aliuliza.