Chelsea yarudi kileleni, Mancity yazuiwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Diego Costa wa Chelsea

Kilabu ya Chelsea imerejea katika uongozi wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuicharaza Newcastle 2-0 katika uwanja wa nyumbani stamford bridge.

Hatua hiyo inajiri baada ya Mancity kuzuiwa na wenyeji wao Everton katika mechi iliokuwa na kasi na mchezo mzuri.

Mancity ndio iliokuwa ya kwanza kufunga kupitia mchezaji wake Fernandinho lakini dakika tatu baadaye mchezaji Naismith wa Everton alisawazisha na kufaya mambo kuwa 1-1.

Matokeo hayo yanaiweka Mancity katika nafasi ya pili ikiwa na alama 47 dhidi ya Chelsea ambayo sasa iko kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na alama 49.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mancity wapata sare ya 1-1 dhidi ya Everton

Katika mechi ya Stamford Bridge Newcastle ambayo ndiyo timu ya kwanza kuifunga Chelsea katika ligi hiyo msimu huu haikuonyesha makali yake kama yale yalioonekana wakati iliposhinda mechi ya awamu ya kwanza.

Chelsea ilipata mabao yake mawili kupitia Oscar na baadaye Diego Costa akawazunguka mabeki wa Newcastle na kufunga bao la pili.

Haya hapa ni matokeo ya mechi za Jumamosi:

Sunderland0 - 1 liverpool FT

Burnley 2 - 1 QPR FT

Chelsea 2 - 0 Newcastle FT

Everton 1 - 1 Man City FT

Leicester 1 - 0 Aston Villa FT

Swansea 1 - 1 West Ham FT

West Brom 1 - 0 Hull FT