Liverpool yaimarisha matokeo yake

Haki miliki ya picha PA
Image caption LIverpool yaibuka mshindi dhidi ya Sunderland

Bao la kipindi cha kwanza lililofungwa na mchezaji Lazar Markovic lilitosha kuipa ushindi Liverpool dhidi ya wenyeji wao Sunderland katika uwanja wa stadium of light.

Licha ya Sunderland kujaribu kufanya mashambulizi katika lango la Liverpool,ni wageni wao ndio waliodhibiti asilimia kubwa ya mechi hiyo huku mchezaji Coutinho akiimarisha safu ya kati na ile ya mashambulizi ya Liverpool.

Liverpool walinyimwa penalty ya wazi katika dakika za kwanza kabla ya Markovic kuwapita walinzi wa Sunderland na kucheka na wavu.