Messi:''Tetesi za kuhama ni porojo tu''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Messi na wachezaji wenzake wa Barcelona

Mchezaji mahiri, Lionel Messi anasema kuwa atasalia katika klabu ya Barcelona baada ya kukanusha umbea wa watu kwamba yuko njiani kutoka Barceola.

Messi ambaye ni mshambuliaji wa Barcelona anasisitiza kwamba hataki kuondoka Barca na kusema madai kwamba alimtaka kocha Luis Enrique, kupigwa kalamu ni porojo tupu.

Taarifa za awali zilisema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alitaka sana kuondoka katika klabu hio kufuatia tofauti kati yake na kocha Enrique.

"sina nia ya kuondoka na kuhamia klabu yoyote kama vile Chelsea au Man City,'' alisema Messi baada ya kuhakikisha timu yake ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Atletico Madrid.

"nimechoshwa sana na umbea wa watu. Sikutaka klabu kumfuta kazi mtu yeyote. ''

Messi, ameteuliwa kuwania tuzo ya mcherzaji bora zaidi duniani, amekuwa akicheza Nou Camp, kwa miaka mingi huku akipata akishinda mataji mengi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Messi akipepea uwanjani

'Messi awajibu wadaku na wambea'

''Watu wanavyoongoea untadhani mimi ndiye mkuu wa klabu. Mimi simuulizi mtu yeyote kufanya uamuzi. Kila kilichosemwa ni uongo mtupu na ningetaka watu kufahamu kwamba madai yote yaliyotolewa ni uongo mtupu. ''

Kulikuwa na tetesi kuwa Messi alikuwa njiani kuondoka Barca, kufuatia taarifa kwamba alitofautiana sana na kocha Enrique, ambaye alichukua usukani wa klabu mwaka jana.

Lakini Messi aliongeza kuwa: ''watu wanasema hizi taarifa kwa lengo la kutuvuruga. Yote haya yananiumiza moyo wangu kwa sababu waliyoyasema hayo ni watu wa Barca. Lazima tuungane. ''

Messi alicheza mchezo wa kufana sana wakati Barcelona walipoicharaza mabingwa watetezi wa La Liga Atletico Madrid.