Kocha bora wa dunia ataka mabadiliko

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Joachim Low

Kocha wa ujeruman Joachim Low ambae ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwaka ametaka mabadiliko .

Low ametaka kuwe kunafanyika mabadiliko ya wachezaji wanne baadala ya watatu wa sasa ili kuleta utamu zaidi katika mchezo wa soka .

"Kama idadi ya wachezaji itaongezwa italeta utamu zaidi katika soka" alieleza kocha huyo wa Ujerumani.

Low aliyeiwezesha Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia nchini Brazil, aliwashinda Diego Simeone na Carlo Ancelotti katika tuzo ya kocha bora wa dunia.