Fainali kombe la mapinduzi kupigwa leo

Image caption Kikosi cha Mtibwa sugar kitakachopambana na Simba.

Michuano ya kombe la mapinduzi kufika tamati leo kwa timu za Simba na Mtibwa kucheza mchezo wa fainali.Fainali hiyo itachezwa katika uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar

Hii itakuwa mara ya pili kwa Timu hizi kukutana kwenye Mashindano haya kwani walikuwa Kundi moja ambapo katika mchezo wa makundi Mtibwa Sugar iliifunga Simba 1-0.

Mchezo huu unaumuhimu kwa pande zote Simba wakihitaji kulipa kisasi cha kuchapwa katika mchezo wa kwanza na kumpa kikombe cha kwanza kocha wao mpya Goran Kopunovic.

Huku Mtibwa wakitaka kuendeleza ubabe wao kwa kuwafunga Simba na kutwaa ubigwa wa kombe la Mapinduzi .

Michuano hii maalumu kwa ajili ya kumbukumbu za mapinduzi ya Zanzibar ilishirikisha jumla ya timu 12.