Patrick Reed atwaa ubigwa wa gofu

Image caption Bingwa wa golf Patrick Reed

Patrick Reed ameibuka bingwa wa mchezo wa gofu katika michezo ya Hyundai iliyofanyika Hawaii kwa kumchapa Jimmy Walker.

Reed mwenye umri wa miaka 24 alikua nyuma ya Walker kwa mipigo minne kabla ya kurudisha kupata ushindi.

Akielezea mchezo huo Reed alisema “"Nilidhani nafasi yangu walikuwa ndogo lakini nilikua na subira na nikashinda ,"

Jason Day wa Austalia alimaliza nafasi ya tatu kwa kupiga mipigo 62 akifunga na Russell Henley wa Marekani na Mjapan Hideki Matsuyama.

Reed,anashikilia nafasi ya 14 katika wiwango vya ubora vya dunia vya mchezo wa gofu.