Wilfried Bony: Ajiunga rasmi City

Image caption Kifaa Bony

Mshambuliaji wa Wilfried Bony amesaini mkataba wa miaka minne unusu kuichezea timu Manchester City wenye thamani ya £28milion.

Bony amekubali mkataba huu na atavaa jezi namba 14iliyokua ikitumiwa na nyota na Javi Garcia.

Baada kusajiliwa na City Bony ameelezea ni "Ni heshima kubwa kuwa hapa na ni changamoto kwangu".

Mchezaji huyo mwenye miaka 26 alitua ligi ya England mwaka 2013 akijiunga na klabu ya Swansea akitokea Vitesse Arnhem ya Uholanzi kwa ada ya uhamisho ya £12milioni na kuwa moja kati ya wafungaji bora katika ligi kuu.

Kwa uhamisho huu unamfanya Bony kuwa mmoja kati ya wachezaji wa Afrika wanaolipwa pesa nyingi duniani katika mchezo wa soka.