Radamel Falcao ataenda wapi msimu ujao?

Haki miliki ya picha PA
Image caption Radamel Falcao kuchezea moja kati ya timu bora msimu ujao

Radamel Falcao atachezea moja kati ya timu bora duniani msimu ujao,hata kama haitakuwa Manchester United, hayo ni maneno ya wakala wa Falcao, Jorge Mendes

Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 28 alitokea Monaco na kujiunga na Man U kwa mkopo mwezi Septemba lakini tangu wakati huo aliifungia Man U magoli matatu pekee.

United wana muda mpaka mwezi June hapo wataamua kama wataendelea naye au la.

Nini maamuzi ya Falcao mwenyewe ?

Falcao mwenyewe ameshaamua kuwa hatarejea Monaco, yaani angependa kubaki United

hata hivyo, akiwa na United Falcao hakuwemo hata kwenye kikosi cha wachezaji 18 walipokutana na Southampton tarehe 11 mwezi huu.

Lois Van gaal amesema uamuzi wake uliegemea kwenye uchaguzi wa wachezaji ambao alihisi kuwa ndio bora zaidi kwa mchezo huo.