Michuano Afrika:Wasiomudu kupewa tiketi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema

Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema , amesema yeye mwenyewe atalipa jumla ya tiketi elfu arobaini kwa ajili ya wapenzi wa soka nchini mwake ili waweze kuhudhuria mechi ya Kombe la Mataifa Afrika.

Michuano hiyo inayoanza jumamosi, yalitangazwa kufanyika nchini humo baada ya kuthibitishwa kuwa hayatafanyika morocco kama ilivyopaswa.

Rais Obiang anasema anaona ni wajibu kwake na wengine wenye uwezo kununua tiketi kufanya hivyo akitoa wito wa kujaza viwanja. Ametoa wito kwa wale wenye uwezo wa kuwasaidia masikini kufanya hivyo