Pacquiao na Mayweather kuzichapa?

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Floyd Mayweather

Lile pambano la masumbwi la uzito wa welterweight linalosubiriwa kwa hamu kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao limeiva.

Fred Sternburg,ambaye ni wakala wa Pacquiao amekanusha taarifa za mfilipino Floyd kukwaana mjini Las Vegas tarehe 2 mwezi .

Lakini wakala huyo alipoongea na BBC alisema mazungumzo bado yanaendelea ingawa wamefikia hatua nzuri na mwelekeo uko wazi.

Bingwa mara nane wa dunia Pacquiao mwenye umri wa miaka 36 ,atakutana na bondia Mmarekani asiye ambaye kumnyuka ufanye kazi uache kazi Mayweather mwenye umri wa miaka 37 wanatajwa kuwa ni mabondia hodari kwa kizazi hiki ambao hawajawahi kuzinyuka.

Mfilipino Pacquiao yeye anamiliki mkanda wa WBO , wakati Mayweather yeye anamiliki na ni mshindi wa mikanda 2 wa WBC na WBA.

Ingawa hawajakubaliana juu ya kupanda ulingoni,lakini kuna sharti ambalo Mayweather amesisitiza kwamba kabla hajapanda ulingoni shurti wakapime damu.