Josh McNary atuhumiwa kwa ubakaji

Image caption Josh McNary

Josh McNary, kutoka timu ya Indianapolis colts ambaye anakamata nafasi ya ulinzi ,anakabiliwa na tuhuma za ubakaji ,makosa ya jinai na shambulio la kudhuru mwili,na hakuna uthibitisho kutoka kwa mtuhumiwa kukubali tuhuma hizo Josh ana umri wa miaka 26.

Msemaji kutoka katika ofisi ya muendesha mashtaka Peg McLeish,alipoulizwa juu ya madai ya mchezaji huyo, amethibitisha madai hayo na kukataa kutoa maelezo zaidi.

Mwaka 2013 Josh alihitimu mafunzo ya jeshi na kujiunga na timu hiyo ya Colts,ambaye anatarajiwa kuichezea timu ya New England siku ya jumapili katika michuano ya AFC .

Timu yake ya Coalts imesema kwamba wanajaribu kutafuta ukweli dhidi ya tuhuma zinazomkabili Josh.

The NFL has faced criticism recently for its handling of serious allegations against players, and penalties have subsequently increased.

Makosa kama hayo yaliwahi kumkabili mlinzi wa nyuma na mchezaji wa timu ya Baltimore Ravens,Ray Rice ambaye aliadhibiwa kukosa michezo miwili kwa kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake ambaye sasa ni mkewe halali.

Adhabu hiyo baadaye iliongezeka na kuwa muda usiojulikana na baadaye akasimamishwa na kupewa adhabu kali lakini baadaye ilimalizwa katika kikao cha usuluhishi.