Ronaldo de Lima kurejea dimbani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ronaldo de Lima anavyoonekana sasa.

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya brazil Ronaldo Luís Nazário de Lima anatarajia kurejea tena dimbani.

De lima ameahidi kupunguza mwili wake kwa mazoezi kwa lengo la kurejea uwanjani kukipiga na timu Fort Lauderdale inayocheza ligi daraja la pili nchi Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari Ronaldo mwenye miaka 38 amesema "kucheza soka lazima uwe na mwili mzuri wa nitajaribu ni changamoto nina uhakika nitaisaidia ligi na timu."

Ronaldo alitwaa ubigwa wa kombe la dunia mara mbili mwaka 1994 na 2002 akiwa na kikosi cha Brazil.

Amewahi kuvitumikia vilabu vya Barcelona, PSV Eindhoven, Inter Milan and Real Madrid kwa mafanikio makubwa sana.