Tottenham,Bradford,Southampton zasonga mbele

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Tottenham

Timu za Tottenham, Bradford na Southampton zilishinda michezo yao ya Marudiano na kuingia Raundi ya 4 ya kombe la FA.

Tottenham, wakiwa kwao dimbani kwao White Hart Lane, waliipiga Burnley 4-2 baada ya kutanguliwa kwa Bao 2-0 kwa mabao ya Sordell na Wallace.

Huku Tottenham wakisawazisha kupita kwa kiungo Paulinho na Capoue. Kabla ya Chiriches na Rose kuwapa ushindi.

Katika Raundi ya 4 Tottenham wataanzia uwanja wa nyumbani kwa kucheza na Leicester City, Januari 24.

Southampton, wakicheza Ugenini, waliibuka na ushindi kwa kuichapa Ipswich Town Bao 1-0 kwa Bao Shane Long, dakika ya 19 ya mchezo.

Bradford City wakipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi Millwal yaliyofugwa na Hanson, Stead, Halliday na Knott.

Michezo ya raundi ya nne itaanza kupigwa Januari 23.