Wageni kupimwa Ebola kombe la Afrika

Haki miliki ya picha AFP

Chama cha soka cha Africa (CAf) kimetangaza kufanyika kwa vipimo vya ugonjwa wa ebola katika michuno ya kombe la Mataifa ya afrika.

Wachezaji viongozi na washabiki wote watakaowasili katika nchi ya Guinea ya Ikweta watafanyiwa uchunguzi ya ugonjwa huo.

Kulingana na taarifa za Caf timu ya kwanza kuwasili nchi humo, Cape Verde walifanyiwa uchunguzi wa afya na itaendelea kufanyika kwa wageni wote wataowasili.

Guinea ya Ikweta imekuwa mwenyeji wa michuano hiyo baada ya Morocco waliokuwa wenyeji kujitoa kwa sababu za maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.