AFCON kutimua vumbi Jan.17

Fainali za michuano ya kombe la Mataifa ya afrika inatarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Guinea ya Ikweta hapo January 17,2015 .

Guinea wanakuwa wenyeji wa michuano hii baada ya Morroco waliokuwa wenyeji kujitoa kwa hofu ya maambukizi ya ugojwa wa ebola.

Mataifa 16 ya Afrika yatashiriki michuano hiyo ambapo imegawanywa katika makundi manne kundi.

Kundi A linaongozwa na wenyeji Guinea ya Ikweta ,Burkina Faso ,Gabon na Congo.

Kundi B Zambia,Tunisia,Cape Verde na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kundi C Ghana Algeria Afrika Kusini Senegal.

Kundi D Ivory Coasty Mali Cameroon Guinea.

Viwanja vitakavyotumika katika michuano ni Nuevo Estadio de Malabo, ulioko mji mkuu wa Malabo, wenye uwezo wa kuchukua Watazamaji 15,250 na uwanja mwingine ni Estadio de Bata, ulioko mjini Bata, wenye kuchukua Watazamaji 37,500.

Viwanja vingine ni-Estadio de Mongomo, na Nuevo Estadio de EbebiyĆ­n.

Jumla ya waamuzi 44 wameteuliwa kuchezesha michuano hiyo.

Kundi D ndio linaoloneka kama kundi la kifo kwa kuwepo vigogo Cameroon na Ivory Coast huku vigogo hao wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa uchampion wa michuano hiyo.

Timu nyingine zinazopigiwa upatu wa kutwaa kombe hilo ni Ghana, Afrika kusini Senegal pamoja na Zambia kutoka na ubora wa vikosi vyao.

Nyota wanaotarajiwa kutamba katika michuano hii ni pamoja na kiungo Yaya Toure, mshambulia Emmanuel Mayuka wa Zambia Papiss Demba Cisse, Eric Choupo-Moting Gervinho. Bernard Parker wa afrika kusini Asamoah Gyan wa Ghana na mshambuliajin Pierre-Emerick Aubameyang

Kukosekana kwa Timu vigogo kama Nigeria ,Misri pamoja na Angola na majina ya wachezaji wakubwa kama Didie Drobga John mikel obi na Mohamed Aboutrika kunaweza kupunguza mvuto wa michuano hiyo.

Libya walitwaa uchampion wa wa Afrika katika michuano iliyopita swali ni nani ataibuka bigwa kwa Mwaka huu?