Mchezaji wa zamani kuwania urais Fifa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sepp Blatter anawania tena urais ukiwa muhula wa tano

Mchezaji wa zamani wa Ufaransa David Ginola atasimama dhidi ya Sepp Blatter kuwania Urais wa shirikisho la kandanda duniani,Fifa.

Ingawa imetangazwa hivyo hakuna uhakika kama Ginola ataendelea na nia yake.

Anahitaji kuungwa mkono na vyama vitano vya soka na kigezo kingine anapaswa kuwa amejihusisha na soka kwa miaka miwili kati ya mitano iliyopita

Ginola mwenye miaka 47 , aliichezea Ufaransa, pia club ya nchi hiyo Paris St Germain kabla ya kujiunga na New Castle United kwa kitita cha Pauni milioni 2.5 mwaka 1995.

Zoezi la Uteuzi wa nafasi ya urais wa fifa litafungwa tarehe 29 mwezi huu.Blatter amekuwa Rais wa Fifa tangu mwaka 1998 anawania muhula wa tano sasa.